Paris,Ufaransa.
BAO la kichwa la kujifunga la mlinzi wa Angers SCO,Issa Cissokho katika dakika ya 91 limeipa Paris Saint-Germain ubingwa wa kombe la ligi (Coupe de France) kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Jumamosi usiku kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali wa uliochezwa kwenye uwanja wa Stade de France.
Ubingwa huo ambao ni wa 11 unaifanya Paris Saint-Germain iwe ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye michuano hiyo ikifuatiwa na Marseille iliyotwaa ubingwa huo mara 10.
0 comments:
Post a Comment