London,England.
MCHILE Alexis Sanchez ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni maji marefu linapokuja suala la kutandaza kambumbu uwanjani hii ni baada ya leo Ijumaa kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Arsenal kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Sanchez mwenye umri wa miaka 28 ameibuka mshindi baada ya kujinyakulia idadi kubwa ya kura zilizopigwa na mashabiki wa klabu hiyo ya jiji la London kupitia mitandao.
Msimu huu Sanchez aliibeba vilivyo Arsenal katika mgongo wake akiibuka kinara katika kufunga mabao pamoja na kutengeneza.
Hilo lilimfanya nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Colocolo,Udinese na Barcelona ashinde mara tano tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu.
0 comments:
Post a Comment