Libreville,Gabon.
DROO ya upangaji wa makundi ya michuano ya mataifa huru Afrika (AFCON) imefanyika usiku huu huko Libreville nchini Gabon ambapo timu 16 zimegawanya katika makundi manne yenye timu nne nne.
Katika droo hiyo wenyeji Gabon wamepangwa kundi A pamoja na mataifa ya Cameroon,Burkina Faso na Guinea-Bissau.
Mabingwa watetezi Ivory Coast wamepangwa kundi C pamoja na mataifa ya Togo, Morocco na DR Congo.Uganda ambao ni wawakilishi pekee toka ukanda wa mataifa ya CECAFA wao wametupwa kundi Ghana,Mali na Misri.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi lake Januari 14,2017 na kufikia tamati Februari 5,2017.
Droo Kamili
Kundi A:Gabon, Cameroon, Guinea-Bissau,Burkina Faso
Kundi B:Algeria, Senegal, Zimbabwe,Tunisia
Kundi C:Ivory Coast, Togo, Morocco, DR Congo
Kundi D:Ghana, Uganda,Misri, Mali
0 comments:
Post a Comment