Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL itaendelea tena leo jioni kwa michezo sita kuchezwa kuchezwa katika viwanja sita vya miji mbalimbali nchini.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Young Africans watakuwa wageni wa Toto Africans huko CCM Kirumba,Mwanza huku matajiri wa jiji la Dar Es Salaam,Azam FC wao wakiwa nyumbani Chamazi Complex kuvaana na Mtibwa Sugar ya Manungu,Morogoro.
Ndanda FC watakuwa nyumbani Nangwanda Sijaona kuwaalika vijana wa Mbeya City kutoka jijini Mbeya.Michezo mitano itachezwa saa 10:00 Jioni isipokuwa ule wa Azam FC wenyewe utachezwa saa 1:00 Usiku.
Ratiba Kamili
Toto Africans vs Young Africans
Ndanda FC vs Mbeya City
African Lyon vs Maji Maji
Ruvu shooting vs Mwadui FC
Tanzania Prisons vs Stand United
Azam FC Vs Mtibwa Sugar FC (1:00) usiku
0 comments:
Post a Comment