728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 15, 2016

    Simba SC bado kileleni yaifumua Kagera Sugar 2-0 Uhuru.


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WEKUNDU wa Msimbazi,Simba SC,wameendelea kukalia kiti cha uongozi wa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya jioni ya leo kuifunga Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba la uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam.

    Mzamiru Yassin alianza kuifungia Simba SC bao la kuongoza katika dakika ya 43 ya mchezo na kufanya Simba SC waende mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

    Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kizuri zaidi kwa Simba SC baada ya kinara wa mabao kwa sasa Shiza Kichuya kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 75 ya mchezo.

    Penati hiyo ilipatikana baada ya Mohammed Ibrahim kuangushwa ndani ya eneo la boksi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba SC bado kileleni yaifumua Kagera Sugar 2-0 Uhuru. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top