728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 13, 2016

    Kiungo wa Everton aingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia


    Liverpool,England.

    KIUNGO wa Everton,Gareth Barry,ameingia katika kitabu cha rekodi za duniani maarufu kama Guinness Book of World Records tolea la 2017 kama mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi ya ligi kuu England akiwa katika kikosi cha kwanza yaani First Eleven.

    Barry,34,ameingia katika rekodi hiyo baada ya kufikisha idadi ya michezo 572 akiwa katika vikosi vya kwanza vya vilabu vya Aston Villa, Manchester City na Everton. 

    Kwa kufikisha idadi hiyo,Barry,amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa muda mrefu na kipa wa zamani wa Liverpool na Portsmouth,David James ya kucheza michezo 571 akiwa kikosi cha kwanza.

    Jumla Barry amecheza michezo 600 ya ligi kuu England akizidiwa pekee na Ryan Giggs anayeshika nafasi ya kwanza na Frank Lampard nafasi ya pili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kiungo wa Everton aingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top