Liverpool, England.
LIVERPOOL imechupa mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu England baada ya usiku huu kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Bromwich Albion katika dimbani la uwanja wa Anfield.
Mabao yaliyoipa Liverpool ushindi katika mchezo huo yamefungwa na Sadio Mane pamoja na Philippe Coutinho katika kipindi cha kwanza.Bao la kufutia machozi la West Bromwich Albion limefungwa na Gareth McAuley.
Ushindi huo umeifanya Liverpool ifikishe pointi 20 na kushika nafasi nafasi ya pili nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment