728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 25, 2016

    Antoine Griezmann mchezaji bora La Liga,Messi,Suarez safi,Ronaldo,Neymar watoka kapa


    Valencia,Hispania.

    MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid na Ufaransa,Antoine Griezmann,usiku wa jana Jumatatu alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi ya Hispania maarufu kama La Liga kwa msimu wa 2015/16 katika sherehe zilizofanyika jijini Valencia.

    Griezmann mwenye miaka 25 ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipokezana tuzo hiyo kwa zamu.

    Tuzo ya kocha bora wa mwaka imeenda kwa kocha wa Atletico Madrid,Diego Simeone huku mshambuliaji wa Barcelona na Uruguay,Luis Suarez,akitangazwa mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wasio raia wa Umoja wa Ulaya akiwabwaga Carlos Kameni,Cedric Bakambu na Faycal Fajr.



    Tuzo Nyingine

    Mshambuliaji bora wa mwaka:Lionel Messi - Barcelona.

    Kipa bora wa mwaka:Jan Oblak - Atletico Madrid.

    Beki bora wa mwaka:Diego Godin - Atletico Madrid.

    Kiungo bora wa mwaka: Luka Modric - Real Madrid.

    Mchezaji bora chipukizi:Marco Asensio - Real Madrid.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Antoine Griezmann mchezaji bora La Liga,Messi,Suarez safi,Ronaldo,Neymar watoka kapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top