Montreal,Canada.
STRAIKA wa zamani wa Chelsea,Didier Drogba,jana Jumapili alitoa mpya baada ya kususa kuichezea klabu yake ya Montreal Impact ya Canada kufuatia kocha wa klabu hiyo Mauro Biello kutomjumuisha kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya klabu ya Toronto FC katika mchezo wa ligi kuu ya Marekani maarufu kama MLS.
Taarifa zilizoifikia SOKA EXTRA zinasema Drogba,38,alikataa katakata kucheza mchezo huo na kuomba jina lake liondolewe kabisa kikosini baada ya kuambiwa kuwa alipaswa kuanzia benchi katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
"Drogba hakuchaguliwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza.Niliongea nae jana (Jumamosi) lakini hakuafiki kuanzia benchi,mwisho alitaka aondolewe kabisa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kilichoandaliwa kwa ajili ya mchezo huo.Amesema Biello.
Biello amedai kuwa alichagua kumwanzisha mshambuliaji wa Italia,Matteo Mancosu,kutokana na kuwa katika hali nzuri kimchezo huku akitumaini kuwa kasi yake ingekuwa kitisho kwa mabeki wa Toronto FC na pindi cha pili angemwingiza Drogba kwenda kumaliza Kazi lakini mpango huo ulikwama baada ya nyota huwa wa Ivory kususa.
0 comments:
Post a Comment