Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI KUU ya vodacom Tanzania Bara (VPL) itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam ambapo vinara wa ligi hiyo Wekundu wa Msimbazi,Simba SC,watakuwa wenyeji wa Mbao FC ya Mwanza.
Simba SC wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 23 katika michezo tisa iliyopita.Ushindi katika mchezo wa leo utaendelea kuwaweka kileleni.
Mbao FC wako nafasi ya kumi na moja baada ya kujikusanyia pointi 12 katika michezo kumi.Ushindi wowote leo utawafanya wafikishe pointi 15 na kuwapandisha mpaka nafasi ya sita.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi Octoba 22 kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa Kagera kuvaana na wenyeji wao Kagera Sugar.
Jumamosi
African Lyon v Mbeya FC
Ndanda FC v Mwadui FC
Mtibwa Sugar v Stand United
Kagera Sugar v Yanga SC
Majimaji FC v Ruvu Shooting
Azam FC v JKT Ruvu
Jumapili
Simba SC v Toto Africans
Tanzania Prisons v Mbao FC
Msimamo
0 comments:
Post a Comment