Ally Mustapha ‘Barthez’
Dar Es Salaam,Tanzania.
KIPA wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’,amefunguka na kumtetea mwenzake, Ally Mustapha ‘Barthez’ kwa kudai kuwa bao alilofungwa kwenye mchezo dhidi ya Simba na winga, Shiza Kichuya, ni bao la kawaida ambalo kipa yeyote anaweza kufungwa.
Dida amesema: “Ni goli la kawaida na lilitokana na makosa tu ya kibinadamu, kama unavyoelewa, hakuna mtu mkamilifu, yalitokea makosa madogo wenzetu wakasawazisha, ndio sehemu ya mchezo,” alisema.
Dida alisema matokeo ya sare ya bao 1-1 waliyoyapata timu yake kwenye mchezo huo dhidi ya Simba, ni sehemu ya mchezo wa soka haswa ikizingatiwa kuwa mpira ni mchezo wa makosa.
Kauli hiyo ya Dida imekuja baada ya mwenzake Barthez kujikuta kwenye lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga kumlaumu kufuatia kutunguliwa Kichuya kutoka kwenye mpira wa kona uliojaa moja kwa moja wavuni katika dakika za lala salama za pambano dhidi ya Simba.
(BINGWA)
0 comments:
Post a Comment