Accra,Ghana.
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana,Black Stars,Malik Jabir,amesema kuzorota/kusuasua na kukosa ushindani kwa ligi kuu ya nchi hiyo kuna sababishwa na wachezaji wa vilabu shiriki kufanya ngono kupita kawaida.
Malik,71,ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Asante Kotoko ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifanya mahojiano na kipindi cha michezo cha redio ya taifa ya Ghana.
Kocha huyo aliyewahi kuifundisha Black Stars mwaka 2003 amesema wachezaji wa ligi kuu ya nchi hiyo wanashindwa kuonyesha Soka safi na ushindani wa kweli kwa kuwa wamekuwa mahodari zaidi kwenye kufanya ngono kuliko kufanya mazoezi na kuboresha viwango vyao.
“Wanafanya sana ngono,hali ambao inaharibu mpaka ubora wa ligi yetu.Hapa Ghana kuna mabinti wengi wazuri na warembo ambao kazi yao ni kula sahani moja na wachezaji.
Wachezaji wanapaswa kufahamu kuwa kuna wakati wa kufanya ngono na kuna wakati wa kucheza mpira.Mchezaji hawezi kufika mbali kama atachanganya mambo yote mawili kwa wakati mmoja.
“Wachezaji wengi wa siku hizi hawana ubavu wa kucheza dakika 90 kwa sababu wanachoka kirahisi mno.Unajua kwanini??Hawalali vya kutosha,hawafanyi mazoezi vya kutosha na wanafanya sana ngono.Wakati mwingine wanafanya ngono hata kabla ya mechi.Alimaliza Malik aliyewahi kuichezea Ghana katika fainali mbili za Olimpiki za mwaka 1968 na 1972.
Malik anakuwa kocha wa pili kukemea ngono kwa wachezaji wa Ghana.Wa kwanza alikuwa ni Mjerumani Berti Vogts ambaye katika miaka ya tisini alipiga marufuku wachezaji wake kufanya ngono kabla ya mechi.
0 comments:
Post a Comment