728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 26, 2016

    VPL:Yanga SC yaigonga JKT Ruvu 4-0,Chirwa atupia tena,Tambwe apiga mbili


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    YANGA SC imeendelea kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu kutoka mkoani Mpwani.

    Obrey Chirwa alianza kuiandikia Yanga SC bao la kuongoza katika dakika ya 5 ya mchezo baada ya kazi nzuri ya Simon Msuva aliyewatoka walinzi wa JKT Ruvu.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

    Kipindi cha Yanga SC iliendelea kutakata kwa kupata mabao matatu zaidi yaliyofungwa na Amissi Tambwe katika dakika ya 63.Simon Msuva katika dakika ya 82 na Amissi Tambwe tena katika dakika ya 92.

    Ushindi huo umeifanya Yanga SC ifikishe pointi 24 baada ya kucheza michezo 11,pointi 5 nyuma ya vinara Simba SC wenye pointi 29.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:Yanga SC yaigonga JKT Ruvu 4-0,Chirwa atupia tena,Tambwe apiga mbili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top