Barcelona,Hispania.
BEKI wa kati wa Barcelona,Gerard Pique,amefichua kuwa atajiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania mara baada ya fainali zijazo za kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika katika ardhi ya Urusi kwa kile anachoamini kuwa kuna baadhi ya watu hawataki kumuona akikitumikia kikosi hicho.
Pique,29,ametoa kauli hiyo leo baada ya jana Jumapili vyombo vya habari na mashabiki wa Hispania kumshutumu vikali kuwa aliondoa kwa makusudi rangi ya bendera ya nchini hiyo pale alipokata mikono jezi yake yenye mikono mirefu na kuwa mifupi katika mchezo wa kundi G wa kusaka tiketi ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Albania ulioisha kwa kikosi chake kushinda kwa mabao 2-0.
Akitoa utetezi wake kabla ya kutoa kauli ya kutaka kujiuzulu,Pique,ambaye amekuwa mstali wa mbele kuunga mkono harakati za jimbo lake la Catalunya kutaka kujiondoa katika nchi ya Hispania amesema alikata mikono ya jezi hiyo kwa kuwa haikumfanya awe huru zaidi uwanjani na si kweli kuwa hataki kuvaa jezi yenye rangi ya bendera ya Hispania.
Huwa ninajitolea kwa kila kitu ninapokuwa uwanjani,lakini kuna watu wanafikiri kuwa ni bora nisiwepo kikosini.Amesema Pique.
Baada ya fainali zijazo za kombe la dunia la mwaka 2018 za nchini Urusi nitajiweka kando na timu hii.
0 comments:
Post a Comment