Atteridgeville,Afrika Kusini.
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imejiweka katika mazingira mazuri ya kutawazwa kuwa machampion wapya wa soka wa Afrika baada ya jioni ya leo kuifunga miamba ya Misri,Zamalek,kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Lucas Moripe huko Atteridgeville,Afrika Kusini.
Mabao yaliyoipa Mamelodi Sundowns ushindi katika mchezo wa leo yamefungwa na Anthony Laffor katika dakika ya 31, Tebogo Langerman katika dakika ya 40 na Percy Tau katika dakika ya 46.
Sasa Mamelodi Sundowns inahitaji ushindi ama sare yoyote ile katika mchezo utakaochezwa wikendi ijayo huko Misri ili iweze kutwaa ubingwa huo ambao msimu uliopita ulitwaliwa na TP Mazembe ya Congo DR.
Vikosi
Mamelodi Sundowns: Onyango; Langerman,Nthethe, Arendse (Soumahoro 70'), Mbekile -Kekana (T. Zwane 85'), Mabunda - Dolly, Tau,Laffor - Billiat (Modise 65')
Zamalek: Elshenawy (Elrehim 63'); Maroof,Eslam Gamal, Al Gabr, Tawfik - Ohawuchi,Ibrahim Salah, Tarek Hamed - Shikabala (Ramzi 55'), Hefny, Morsy (Mohamed Fathi 76')
0 comments:
Post a Comment