London,England.
MABAO mawili ya kipindi cha kwanza ya Diego Costa na Eden Hazard na bao moja la kipindi cha pili la Mnigeria,Victor Moses,yameipa Chelsea ushindi wa mabao 3-0 nyumbani Stamford Blidge dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu England, Leceister City,mchana wa leo.
Diego Costa alianza kuifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 6 ya mchezo akiuwahi mpira wa kisigino wa kiungo Nemanja Matic.Eden Hazard alifunga bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Pedro Rodriquez na kufanya Chelsea iende mapumziko ikiwa mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.
Kipindi cha pili ilikuwa ni Chelsea tena walioendelea kutabasamu baada ya Victor Moses kufunga bao la tatu kwa mkwaju wa karibu akimalizia pasi ya kisigino toka kwa Nadhaniel Chalobah.
0 comments:
Post a Comment