Alexandria, Misri.
MAMELODI Sundowns ya Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa ufalme wa michuano ya klabu bingwa Afrika kwa mwaka 2016 licha ya Jumapili Usiku kuchapwa bao 1-0 na Zamalek ya Misri katika mchezo wa fainali ya pili ya michuano hiyo uliochezwa katika uwanja wa Borg El-Arab Stadium huko Alexandria, Misri.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakika ya 64 na Stanley Ohawuchi kwa mkwaju wa mbali wa mita 30 uliomshinda mlinda mlango wa Mamelodi Sundowns,Wayne Sandilands na kutinga wavuni.
Matokeo hayo yameifanya Mamelodi Sundowns kuwa mabingwa kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Afrika Kusini wiki moja iliyopita Mamelodi Sundowns ilishinda kwa mabao 3-0.
Mamelodi Sundowns inakuwa klabu ya pili ya Afrika Kusini kutwaa ufalme wa soka Afrika baada ya ndugu zao Orlando Pirates kufanya hivyo mwaka 1995.
Vikosi:
Zamalek: Genesh, Youssef, Dowidar, Gabar,Khaled (Shikabala 76’), Fathi, Hamed (Salah 85’), Tawfik, Stanley, Hefny (Mayuka 85’),Morsy.
Sundowns: Onyango (Sandilands 28’), Mbekile,Soumahoro, Nthethe, Langerman, Kekana,Mabunda, Tau, Dolly, Billiat (S. Zwane 84’),Laffor (Modise 72’).
0 comments:
Post a Comment