Nice,Ufaransa.
KLABU ya OGC Nice inayochezewa na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia,Mario Balotelli,imeendelea kukalia kiti cha uongozi wa ligi daraja la kwanza Ufaransa,Ligue 1,baada ya Ijumaa usiku ikiwa nyumbani Stade Riviera kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lyon.
Paul Baysse alianza kuifungia OGC Nice bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo akimalizia mkwaju wa Younes Belhanda uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.
Nabil Fekir wa Lyon akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Jean-Michael Seri aliihakikishia OGC Nice kuondoka na alama zote tatu baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya 76 ya mchezo.Mario Balotelli alishindwa kuendeleza kasi yake ya kupachika mabao tangu ajiunge na OGC Nice akitokea Liverpool baada ya kukosa mkwaju wa penati katika dakika ya 81 ya mchezo.
OGC Nice maarufu kama The Azurean sasa wana alama 23 baada ya kushuka dimbani mara tisa,alama nne zaidi ya wanaoshika nafasi ya pili Monaco, ambao katika mchezo uliochezwa mapema walikutana na kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Toulouse.
0 comments:
Post a Comment