Gibraltar
MSHAMBULIAJI wa Ubelgiji,Christian Benteke,ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga bao la mapema zaidi katika michezo inayohusisha timu za taifa baada ya Jumatatu Usiku kufunga bao la sekunde ya saba (7) katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Gibraltar kwenye mchezo wa kundi H wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia.
Benteke alifunga bao hilo baada ya kuunasa mpira uliokuwa umeguswa na wachezaji wawili tu wa Gibraltar kisha kukimbia kwa kasi golini na kufunga.
Bao hilo limevunja rekodi ya bao jingine la mapema zaidi lililofungwa na Davide Gualtieri wa San Marino ,Novemba 17, 1993 pale alipofunga bao la sekunde ya nane (8.3) dhidi ya England katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment