728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 14, 2016

    Rashford amtaja beki mgumu zaidi kuwahi kukutana nae

    Manchester,England.

    STRAIKA kinda wa Manchester United,Mwingereza,Marcus Rashford amemtaja nahodha msaidizi wa Arsenal,Mfaransa Laurent Koscielny kuwa ndiye beki mgumu zaidi aliyewahi kukutana nae katika maisha yake ya soka.

    Akifanya mahojiano na kipindi cha Football & Me kinachoendeshwa na mtandao wa Manchester United,Rashford,19,amesema ameshakutana na mabeki wengi wagumu tangu alipoanza kuichezea Manchester United mwezi Februari mwaka huu lakini Koscielny,31,ndiye mwisho wa matatizo.

    Koscielny alijiunga na Arsenal Julai 2010 kwa ada ya £11m akitokea FC Lorient ya nyumbani kwao Ufaransa.Mpaka sasa ameshaichezea Arsenal jumla ya michezo 256 na kuifungia mabao 22 na anatajwa kuwa mmoja kati ya mabeki bora zaidi wa kati kwa sasa duniani.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Rashford amtaja beki mgumu zaidi kuwahi kukutana nae Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top