Cordoba,Argentina.
IKICHEZA nyumbani Cordoba,Argentina, imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Paraguay katika mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia kwa mataifa ya Amerika Kusini maarufu kama CONMEBOL.
Argentina ambayo ilimkosa staa wake Lionel Messi,anayesumbuliwa na majeruhi ilijikuta njia panda dakika ya 18 ya mchezo baada ya Derlis Gonzalez kuifungia bao la kuongoza akimalizia pasi safi ya Angel Romero.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wenyeji Argentina ambao walikuja juu kama moto wa kifuu lakini juhudi zao zilizimwa na safu imara ulinzi ya Paraguay iliyokuwa ikiongozwa na mlinda mlango Justo Villar aliyekuwa shujaa kwa kucheza penati ya Sergio Aguero.
Katika mchezo mwingine Brazil ikicheza ugenini Merida imewachapa wenyeji wao Venezuela kwa jumla ya mabao 2-0 yaliyofungwa na Gabriel
Jesus pamoja na Willian.
Colombia ikiwa nyumbani Barranquilla imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 Uruguay.Mabao ya Colombia yamefungwa na Abel Aguilar pamoja na Fernando Mina.Mabao ya Uruguay yamefungwa na Cristian Rodriguez pamoja na Luis Suarez.
Chile imeichapa Peru kwa mabao 2-1.Shukrani kwa mabao ya Arturo Vidal aliyefunga mara mbili. Bao la Peru limefungwa na Edison Flores.
Ecuador imefungana mabao 2-2 na Bolivia. Mabao yote ya Ecuador yamefungwa na Enner Valencia huku Pablo Escobar akifunga mabao yote ya Bolivia.
0 comments:
Post a Comment