Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imeendelea tena leo Jumatano kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Yanga ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru imeichapa Mtibwa Sugar toka Manungu,Morogoro, kwa mabao 3-1.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Obrey Chirwa dakika ya 45,Simon Msuva dakika ya 68 na Donald Ngoma dakika ya 80 akimalizia kazi safi ya Geoffrey Mwashiuya. Bao la Mtibwa Sugar limefungwa na Haruna Chanongo dakika ya 63.
Vinara wa ligi hiyo Simba wameichapa Mbeya City kwa jumla ya mabao 2-0 huko katika dimba la uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mabao ya Simba yamefungwa na Ibrahim Ajib kwa mpira wa adhabu pamoja na Shiza Kichuya kwa mkwaju mkali baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Mbeya City.
Stand United ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kambarage imeichapa Azam FC kwa bao 1-0 lililofungwa na Adam Salamba.
Matokeo Mengine
Mbao FC 2 -0 Toto Africans
Stand United 1-0 Azam FC
Mwadui FC 2-0 African Lyon.
Majimaji FC 0-1 Kagera Sugar
JKT Ruvu 0-0 Tanzania Prisons
0 comments:
Post a Comment