Milan,Italia.
GRAZIANO PELLE ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia baada ya kukataa kushikana mikono na Kocha wake Giampiero Ventura wakati akifanyiwa mabadiliko [Substitution].
Pelle,31,alifanya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu Alhamisi Usiku (Jana) pale alipotolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Ciro Immobile katika mchezo ambao Italia ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kundi F wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia.
Taarifa kutoka katika tovuti rasmi ya chama cha soka cha Italia imesema tayari Pelle ameshapandishwa ndege kurudishwa katika klabu yake ya Shandong Luneng inayoshiriki ligi kuu ya China.
Hii ina maana kwamba Pelle hatakuwa sehemu ya kikosi cha Italia ambacho siku ya Jumapili kitakuwa ugenini Skopje kuvaana na FYR Macedonia katika mchezo mwishine wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment