Madrid,Hispania.
HATARI!!Real Madrid imenogewa na huduma za staa wake kutoka Wales,Gareth Bale na katika kuonyesha kuwa imekufa kwa mkali huyo anayejua vyema kuutumia mguu wake wa kushoto tayari imemuandalia mkataba mpya na mnono wa miaka sita.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kituo cha Radio Cadena Ser cha Hispania,mkataba huo mpya utamfanya Bale,27,aendelee kubaki Santiago Bernabeu mpaka mwishoni mwa msimu wa 2021-22.
Aidha katika mkataba huo mpya Real Madrid imeweka kipengele cha kumuuza mkali huyo wa zamani wa Tottenham kwa ada ya uhamisho ya Euro Milioni 500 (Paundi 427)
0 comments:
Post a Comment