Stockholm,Swedeni.
SWEDEN ikicheza katika dimba lake la nyumbani la Friends Arena tena mbele ya mashabiki wake lukuki imeibanjua Wales kwa mabao 3-0 katika mchezo mkali wa kimataifa wa Kirafiki wa kujiandaa na michuano ya Euro 2016 itakayofanyika huko Ufaransa kuanzia Juni 10 mwaka huu.
Mabao yaliyoifanya Swedeni itoke kifua mbele katika mchezo wa leo yamefungwa na Mikael Lusting dakika ya 40.Emil Forsberg dakika ya 67 na Johan Guidetti dakika ya 86.
Katika mchezo huo kocha wa Wales Cris Coleman alimuweka benchi staa wa timu hiyo Gareth Bale kabla ya kumuingiza dakika za mwisho kutokana na kukabiliwa na uchovu wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment