Rabat,Morocco.
MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi iliendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo miwili ya Kundi A na B kuchezwa.
Kutoka Kundi A, Zesco United ikiwa ugenini huko Rabat,Morocco imefungwa mabao 2-0 na Wydad Casablanca katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Stade Mouray Abdellah.
Mabao ya Wydad Casablanca yamefungwa dakika za 19 na 52 kupitia kwa Walid Karti aliyefunga kwa kichwa na David Owino aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Reda Hajhouj.
Kwa matokeo hayo Wydad Casablanca imezidi kujikita kileleni mwa kundi A baada ya kufikisha pointi sita Zesco United imeshuka kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya tatu ikibaki na pointi zake tatu.Nafasi ya pili inakaliwa na ASEC Mimosas yenye pointi tatu na wastani mzuri wa mabao.Al Ahly ni ya mwisho ikiwa haina pointi yoyote.Timu zote zimecheza michezo miwili.
Kutoka Kundi B,Enyimba International FC ya Aba,Nigeria imeangukia pua kwa mara nyingine baada ya kupoteza mchezo wake wa pili kufuatia kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Mamelodi Sundowns katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Lucas Moripe Stadium huko Pretoria,Afrika Kusini.
Mabao ya Mamelodi Sundowns yamefungwa dakika za 43 na 79 kupitia kwa Leonardo Castro na Wayne Arendse huku lile la Enyimba International likifungwa na Oluwadamidare Ojo dakika ya 59.
Kwa matokeo hayo Enyimba inaendelea kujikalia mkiani mwa kundi B lenye timu tatu hii ni baada ya ES Setif kutolewa mashindanoni.Katika mchezo wa kwanza Enyimba ikiwa nyumbani Aba ilifungwa bao 1-0 na Zamalek ya Misri inayoshika nafasi ya pili.Mamelodi Sundowns wako kileleni kwa wastani wa mabao ya kufunga.
0 comments:
Post a Comment