Adams na Henry.
London,England.
NAHODHA na Mlinzi wa zamini wa Arsenal,Muingereza,Tony Adams,amekubali kurejea tena klabuni hapo lakini safari hii akiwa kama mmoja wa makocha wa kikosi cha vijana cha U-18 .
Adams,49,ambaye amekuwa nje ya ukufunzi/ukocha wa soka tangu mwaka 2011 baada ya kuhudumu katika vilabu vya Wycombe, Portsmouth na Gabala ya Azerbaijani amekubali kurejea baada ya kutakiwa kufanya hivyo na waajiri wake hao wa zamani.
Taarifa kutoka gazeti la The Sun zinasema Adams ataungana na nyota mwingine wa zamani wa klabu hiyo,Thierry Henry kuwa makocha wasaidizi wa kikosi hicho kitakachokuwa chini ya Kocha Mkuu, Kwame Ampadu ambaye pia aliwahi kuichezea Arsenal.
Adams ambaye alikuwa mmoja kati wa walinzi mahiri wa klabu hiyo amerejeshwa ili kusaidia kuijenga upya safu ya ulinzi ya kikosi hicho ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa na mapungufu makubwa kiasi cha kutishia ushiriki wake katika michuano mbalimbali ya vijana.
Akiwa na Arsenal,Adams alifanikiwa kucheza michezo 674 akishinda mataji manne ya ligi kuu England,mataji matatu ya FA Cup,mataji mawili ya kombe la ligi (Carling Cup) na taji la washindi Ulaya maarufu kama Cup Winners’ Cup ambalo kwasasa linaitwa Europa Ligi.
0 comments:
Post a Comment