Sekondi-Takoradi,Ghana.
Medeama FC ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Essipong Sports Stadium huko Sekondi-Takoradi imelazimishwa sare ya bila kufungana na MO Bejaia ya Algeria katika mchezo mkali wa Kundi A wa kombe la shirikisho Afrika uliochezwa jioni ya leo.
Mpaka dakika 90 zinakwisha hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuliona lango la mwenzie
Kwa matokeo hayo Medeama FC imefikisha alama moja baada ya kucheza michezo miwili.Katika mchezo wa kwanza Medeama FC ilifungwa mabao 3-1 na TP Mazembe huko Lubumbashi.Mo Bejaia wao wamefikisha alama nne baada ya kucheza michezo miwili.Katika mchezo wao wa kwanza waliifunga Yanga kwa bao 1-0.
Timu hizo zitarejea tena dimbani mwezi ujao ambapo Medeama FC watasafiri mpaka Dar es Salaam kucheza na Yanga Julai 15 wakati Mo Bejaia wao watakuwa wageni wa TP Mazembe huko Lubumbashi Julai 17.
0 comments:
Post a Comment