Stockholm, Sweden.
SASA ni Rasmi kuwa Zlatan Ibrahimovic atajiunga na Manchester United kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England na Michuano mingine ikiwemo Europa Ligi,Capital One na FA Cup.
Staa huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 34 atafanyiwa vipimo vya afya yake kesho Ijumaa na siku hiyo hiyo atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Manchester United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kurefushwa kwa mwaka mmoja zaidi.
Je,Kwanini tangazo la kujiunga na Manchester United limetoka leo?
Tangazo hilo limetoka leo Juni 30 kwa kuwa leo ndiyo siku ambayo mkataba wa Ibrahimovic na iliyokuwa klabu yake ya Paris Saint Germain umefikia mwisho.
Tayari wadadisi wa Masuala ya Kimichezo wameshaanza kubashiri namna ambavyo kikosi cha Manchester United chini ya Mreno Jose Mourinho kitakavyokuwa msimu ujao wa 2016/17.
UBASHIRI HUU HAPA!!
0 comments:
Post a Comment