New Jersey,Marekani.
Lionel Messi ametangaza kustaafu kuichezea Argentina baada ya kuishuhudia timu hiyo ikipoteza fainali ya pili ya Copa America kwa kufungwa kwa penati 4-2 na Chile katika mchezo wa fainali uliochezwa Alfajiri ya leo huko New Jersey,Marekani.
Messi,29,amechukua uamuzi huo baada ya kupoteza jumla ya fainali nne akiwa na Argentina ambapo kati ya hizo tatu zimefuatana hali ambayo imemsononesha sana na kujiona kuwa ni mtu mwenye bahati mbaya na timu hiyo.
Messi alianza kupoteza fainali ya kwanza mwaka 2007 ambapo Argentina ilipoteza mchezo wa fainali ya Copa America kwa kufungwa na Brazil kwa mabao 3-0.Mwaka 2014 Argentina ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani katika fainali ya Kombe la dunia.Fainali za Copa America za 2015 na 2016 dhidi ya Chile zote kwa mikwaju ya penati
Messi amesema "Imetosha sasa kuichezea Argentina.Nimefanya kila nilichoweza,inauma kushindwa kuwa bingwa.Fainali nne,zote nimeshindwa imetosha sasa.Nimejaribu,Nimeshindwa kupata nilichokihitaji.
Taarifa zaidi kutoka kambi ya Argentina zinadai mbali ya Messi ambaye tayari ametangaza kustaafu nyota wengine wa timu hiyo Javier Mascherano, Lucas Biglia, Ever Banega, Ezequiel Lavezzi na Angel Di MarÃa nao wako njiani kubwaga manyanga kuichezea Albiceleste.
0 comments:
Post a Comment