728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 29, 2016

    KUELEKEA MSIMU MPYA WA VPL:MBEYA CITY,STAND UNITED ZATEMA WACHEZAJI KUMI NA NNE

    Dkt.Ellyson Maeja.

    Mbeya,Tanzania.

    VILABU vya Mbeya City ya jijini Mbeya na Stand United ya mkoani Shinyanga kwa pamoja vimetangaza kutema wachezaji kumi na nne katika vikosi vyao vya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    Mbeya City kupitia kwa Katibu wake Mkuu,Emmanuel Kimbe imetangaza kutema wachezaji saba.Wachezaji hao ni Mlinda mlango, Haningtony Kalyesubula, Walinzi ni Yusuph Abdalah Sisalo, Deo Julius, Hamad Kibopile, Yohana Morris, Richard Peter Chundu na Mshambualiaji Temmi Felix.

    Akitoa sababu ya klabu yake kuamua kuachana na wachezaji hao,Kimbe amesema kuwa wachezaji hao wameshamaliza mikataba yao na hivyo Mbeya City imeridhia kuachana nao ili wasake timu nyingine mapema.

    Kwa upande wa Stand United jumla ya wachezaji saba wameonyeshwa mlango wa kutokea na klabu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Acacia.Mwenyekiti Mpya wa klabu hiyo Dkt. Ellyson Maeja amewataja wachezaji hao kuwa ni Haruna Chanongo,Abuu Ubwa,Nasoro Masoud
    Chollo,Hassan Seif Banda,Elius Maguli na Philip Methusela.

    Akitangaza uamuzi huo, Maeja amesema Stand United imeamua kuachana na wachezaji hao kutokana baadhi yao kumaliza mikataba yao na wengine kujisajili na timu za nje.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA MSIMU MPYA WA VPL:MBEYA CITY,STAND UNITED ZATEMA WACHEZAJI KUMI NA NNE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top