728x90 AdSpace

Saturday, June 25, 2016

BALE NA WALES YAKE WATINGA ROBO FAINALI EURO 2016

Paris,Ufaransa.

WALES imekuwa timu ya pili kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya Usiku wa Leo kuifunga Ireland Kaskazini kwa bao 1-0 katika mchezo Mkali uliochezwa katika Uwanja wa Parc des Princes, Paris.

Bao pekee la mchezo huo limepatikana dakika ya 75 baada ya mlinzi wa Ireland Kaskazini, George Mcauley kujifunga wakati akijaribu kuzuia krosi ya winga wa Wales, Gareth Bale toka Magharibi mwa Uwanja.

Kwa matokeo hayo Wales sasa icheza Robo Fainali na mshindi kati ya Hungary ama Ubelgiji.

VIKOSI

WALES XI: Hennessey; Gunter,Chester, A. Williams, Davies, Taylor; Allen,
Ledley, Ramsey; Bale, Vokes

NORTHERN IRELAND XI: McGovern;Hughes, McAuley, Cathcart, J. Evans; C.Evans; Ward, Norwood, Davis, Dallas; Lafferty

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BALE NA WALES YAKE WATINGA ROBO FAINALI EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown