728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 22, 2016

    BURE KABISA:TAKWIMU ZAONYESHA PETER CECH NDIYE KIPA MBOVU ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MICHUANO YA EURO

    Paris,Ufaransa.

    MAMBO hayawezi kuwa sawa muda wote.Kuwa sawa sehemu zote.Hili limejidhihirisha pia kwa Kipa Mkongwe wa Jamhuri ya Czech na Arsenal, Peter Cech.

    Wakati msimu uliopita akiibuka kuwa kipa bora wa wa Ligi Kuu England,akitamba katika vilabu vya Chelsea na baadae Arsenal,Upande wa pili wa shilingi yaani katika timu yake ya taifa, Cech ameendelea kuweka rekodi mbovu zaidi labda hiyo inaweza pia kuwa imechangiwa na ubovu wa timu yake ya taifa ya Jamhuri ya Czech.

    Jana Jumanne Jamhuri ya Czech ilitupwa nje ya michuano ya Euro baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Uturuki katika mchezo wa mwisho wa Kundi D. Jamhuri ya Czech imefungasha virago baada ya kuambulia Alama moja pekee katika michezo mitatu waliyocheza huku wakifunga mabao mawili na kufungwa mabao matano. 

    Kichapo hicho kimemfanya Peter Cech,34, kuwa amefungwa jumla ya mabao 21 katika Fainali za Michuano ya Euro ikiwa ni mabao mengi zaidi kwa kipa mmoja kufungwa katika historia ya Michuano hiyo mikubwa zaidi Ulaya.

    Cech alianza kuichezea Jamhuri ya Czech mwaka 2004.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BURE KABISA:TAKWIMU ZAONYESHA PETER CECH NDIYE KIPA MBOVU ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MICHUANO YA EURO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top