Paris,Ufaransa.
KOCHA wa England, Roy Hodgson anatarajiwa kufanya mabadiliko ya wachezaji sita katika kikosi chake kitakachoshuka dimbani Jumatatu ya leo kuvaana na Slovakia katika mchezo mkali wa Kundi B wa michuano ya Ulaya/Euro 2016.
Hodgson amefikia hatua hiyo ili ili kuhakikisha kikosi chake kinanyakua uongozi wa Kundi hilo lenye mataifa ya Wales,Slovakia na Urusi.
Vyombo mbalimbali vya habari vya England ikiwemo Guardian na Sky Sports News, vimeripoti kuwa nahodha wa kikosi hicho Wayne Rooney ambaye katika michezo miwili ya kwanza dhidi ya Urusi na Wales amekuwa akitumiwa kama kiungo ataanzia benchi na nafasi yake itachukuliwa na Jordan Henderson huku Jack Wilshere akianza badala ya Dele Alli.
Nathaniel Clyne na Ryan Bertrand watachukua nafasi za Kyle Walker na Danny Rose kama mabeki wa kulia na kushoto.
Daniel Sturridge na Jamie Vardy wanatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza wakiwa kama washambuliaji badala ya Harry Kane na Raheem Sterling.
KIKOSI KAMILI KIKO KAMA IFUATAVYO
0 comments:
Post a Comment