728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 22, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JIONI YA LEO JUNI 22,2016

    Paulo Dybala

    Lukaku:Wakala wa mshambuliaji Romelu Lukaku aitwaye Mino Raiola ameiambia AC Milan kuwa haina ubavu  wa kumnunua mteja wake kwasasa labda mpaka hapo itakapokuwa imepata mwekezaji mpya.Raiola amesema Lukaku anapatikana kwa dau kubwa sana,AC Milan na vilabu vingine vya Italia haviwezi kuimudu bei yake. (Sportwereld)

    Chilwell:Mabingwa wa Ligi Kuu England,Leicester City wamekiri kupokea na kuikataa ofa ya £7m iliyoletwa na Liverpool kwa ajili ya kutaka kumsajili beki wake wa kushoto Ben Chilwell,19.Leicester City wanataka wapewe £10m kwa ajili ya beki huyo ambaye bado hajacheza hata mchezo mmoja wa Ligi Kuu.(Liverpool Echo)

    Dybala:Barcelona imedaiwa kuwa itamsajili mshambuliaji wa Juventus,Muargentina Paulo Dybala,22, ikiwa staa wake Neymar Jr ataamua kujiunga na Paris Saint-Germain katika kipindi hiki cha usajili.(Mundo Deportivo)

    Shaarawy: Roma imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji Stephan El Shaarawy,23, kutoka AC Milan kwa ada ya £10m baada ya kuonyesha kiwango kizuri wakati akiwa klabuni hapo kwa mkopo wa msimu mmoja.(Gazetta dello Sport)

    Santos:Arsenal imeripotiwa kufanya mawasiliano na Atletico Mineiro ili kuangalia uwezekano wa kutaka kumsajili beki wa kushoto wa klabu hiyo Douglas Santos.Santos,22,aliyejiunga na Mineiro mwaka 2015 akitokea Udinese kwa dau la £2.5m kwasasa anapatikana kwa dau la £7.7m.(Hoje em Dia)

    Aboubakar:Everton imeanza mazungumzo Rasmi na FC Porto kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mcameroon, Vincent Aboubakar,24,mwenye thamani ya £16m.(The Daily Mail)

    Jesus:Manchester United imetuma ofa ya £15m kwenye Palmeiras ili kujaribu kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Gabriel Jesus. Jesus,19,ameifungia Palmeiras mabao 20 katika michezo 60.

    Sneijder:Meneja wa Everton, Ronald Koeman anataka kukiimarisha kikosi hicho kwa kumsajili kiungo wa Galatasaray, Mholanzi Wesley Sneijder.Msimu uliopita Sneijder,32,aliifungia Galatasaray mabao matano na kutengeneza mengine sita.Anaweza kupatikana kwa ada ya £5.8m.( Express)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JIONI YA LEO JUNI 22,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top