Ahmed El-Shenawy
El-Shenawy:Chelsea imeripotiwa kutaka kutoa kitita cha £3m ili kumsajili kipa wa Zamalek ya Misri,Ahmed El-Shenawy kwa lengo la kumfanya kuwa kipa chaguo la pili baada ya Asmir Begovic kuonyesha nia ya kutaka kuondoka Stamford Bligde.(The Sun)
Zola:Klabu ya Al-Arabi ya Qatari imemtimua kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu,Gianfranco Zola,50,baada ya kujikuta ikimaliza ligi ikiwa nafasi ya nane kati ya timu 14.Nafasi ile ile na pointi zile zile ilizozipata msimu uliopita.Nafasi ya Zola itachukulia na Gerardo Pelusso wa Uruguay.Pelusso atakuwa Kocha wa 13 kujiunga na timu hiyo katika kipindi kisichozidi miaka sita.(Gazzetta)
Puel:Southampton inakaribia kumtangaza kocha wa zamani wa Nice,Claude Puel, kuwa kocha wake mpya.(PA Sport)
Brown:Beki wa zamani wa Manchester United na Sunderland,Wes Brown,36, ameanza kufanya mazoezi na klabu ya daraja la kwanza ya Blackburn Rovers ili kuangalia uwezekano wa kuichezea msimu ujao.(Mirror)
Giggs:Ndoto ya winga wa zamani wa Manchester United,Ryan Giggs kuwa Kocha wa Nottingham Forest imepotea baada ya Klabu hiyo wa London kumtangaza Philippe Montanier kuwa Kocha wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili.(Daily Mail)
Witsel:Vilabu vya Everton na Manchester United vimekwaa visiki katika mbio za kumuwania kiungo wa Ubelgiji, Axel Witsel,26,baada ya wawakilishi wa staa huyo wa Zenit kudai kuwa mteja wao atahamia katika vilabu vinavyocheza ligi ya Mabingwa Ulaya pekee.(Kicker)
Alves:Dani Alves amefaulu vipimo vya afya Juventus na wakati wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Turin.Mkataba huyo utakaokuwa na kipengele cha kurefushwa kwa mwaka mmoja zaidi utamuwezesha Alves,33,kuvuna mshahara wa €3.5m kwa mwaka.(BST)
Barbosa:Mshambuliaji wa Brazil na Santos,Gabriel Barbosa ameonyesha kufurahishwa na mpango wa kujiunga na Arsenal baada ya klabu hiyo ya London kutuma ofa ya £15m ili kumsajili.Barbosa,19,ameifungia Santos mabao 50 katika michezo 150.(ESPN Brazil)
0 comments:
Post a Comment