728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 28, 2016

    YANGA SC YAENDELEZA UNYONGE SHIRIKISHO YACHAPWA 1-0 NA TP MAZEMBE U/TAIFA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    YANGA SC imeendelea kugawa pointi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa TP Mazembe ya DRC katika mchezo mkali wa kundi A uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Bao lililoipa TP Mazembe pointi tatu limefungwa dakika ya 74 na Mereveille Boppe na kuifanya timu hiyo ya Lubumbashi kuendelea kukalia kiti cha Uongozi wa Kundi A baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kushuka dimbani mara mbili.

    Yanga SC haina pointi yoyote mpaka sasa baada ya kucheza michezo miwili na kupoteza yote.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAENDELEZA UNYONGE SHIRIKISHO YACHAPWA 1-0 NA TP MAZEMBE U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top