Nice,Ufaransa.
KATIKA hali isiyotarajiwa Mlinzi wa Hispania,Gerard Pique amejikuta akichapwa Kofi kali la shavuni na Iker Casillas kufuatia kumkosakosa kumpiga tobo kipa huyo wa zamani wa Real Madrid.
Tukio hilo limetokea Jana Ijumaa wakati wachezaji wa Hispania/La Roja walipokuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa hatua ya 16 bora dhidi ya Italia.
Japo Casillas alifaulu kukwepa fedheha ya kupigwa tobo hilo kwa kuwahi kubana miguu yake lakini jaribio hilo la Pique lilionekana kumkera Kipa huyo mkongwe na kuamua kujibu mapigo kwa kurusha kofi kali lililompata sawia Pique na kumfanya ahamaki na kutaka kulipiza lakini wachezaji wenzao waliingia kati na kutuliza hali ya mambo.
0 comments:
Post a Comment