728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 26, 2016

    BREEL EMBOLO AITOSA MAN UNITED NA  KUTUA UJERUMANI KWA $ 28M


    GELSENKIRCHEN,UJERUMANI.

    VILABU vya Manchester United na Tottenham vimeangukia pua katika mbio zake za kumuwania Mshambuliaji wa FC Basel 1893,Breel Embolo baada ya Staa huyo wa Uswisi leo kujiunga na Schalke 04 ya Ujerumani kwa mkataba wa miaka mitano.


    Embolo,19, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Uswisi kilichotupwa nje ya Michuano ya Euro 2016 jana Jumamosi baada ya kufungwa na Poland kwa penati 5-4 amesaini kuichezea Shalke 04 baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kutoa $ 28m na kumpa mkataba utakaofikia Mwisho Juni 30, 2021.

    Emboli anaiacha FC Basel 1893 akiwa ameifungia mabao 20 katika michezo 56 huku akiiwezesha kutwaa vikombe vitatu vya Ligi Kuu ya Uswisi.

    Shalke 04 imemsaini Embolo ili kuongeza makali katika kikosi chake ambacho msimu uliopita kilimaliza nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi ya Bundesliga baada ya kujikusanyia pointi 52 katika michezo 34.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BREEL EMBOLO AITOSA MAN UNITED NA  KUTUA UJERUMANI KWA $ 28M Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top