STRAIKA wa kimataifa aliyemaliza mkataba Azam FC, Didier Kavumbagu,
amenyoosha mikono na kueleza wazi kwamba wachezaji kutoka nje ya nchi
wanaokuja kucheza soka Tanzania, wanatakiwa kuwa na moyo wa chuma.
Akizungumza jana, Kavumbagu alisema wachezaji kutoka nchini
Burundi ni miongoni mwa wahanga ambao wameshindwa kufanya vizuri katika
baadhi ya klabu ikiwemo Simba.
Wachezaji waliotoka nchini humo na kushindwa kucheza kwa muda mrefu
ni Gilbert Kaze, Pierre Kwizera na Kelvin Ndayisenga ambao walishindwa
kufanya vizuri kisha kutimka.
“Ligi ya Tanzania ni tofauti na Burundi, ni lazima kuwa na moyo
mgumu vinginevyo huwezi kufanya kazi kwani kuna matatizo makubwa ndani
na nje ya uwanja yanasumbua ambayo yamekuwa ni kikwazo kwa wachezaji
wengi kutofanikiwa,” alisema.
Kavumbagu amemaliza mkataba na timu hiyo ambapo kwa sasa yupo nchini
Burundi kusikilizia ofa kutoka timu za Mbeya City ya Tanzania, Qatar na
nchini Vietnam.
CHANZO:DIMBA
0 comments:
Post a Comment