Siku chache zilizopita mchezaji wa zamani wa Gary Lineker kwenye Twitter yake aliikashfu Puma kwa kusema, “Jezi za timu ya Uswis zinachanika kama karatasi. Mipira ya Adidas inapasuka. Huwezi kuwekea dhamana bidhaa za Kijerumani!”
Baada ya kashfa hiyo kubwa, kupitia msemaji wao Kerstin Neuber, Puma wameamua kujitokeza hadharani na kusema, “Timu nyingine 5 ambazo zinatumia jezi zetu zimecheza mechi zilizopita bila ya suala hili kutokea. Waataamu wetu wa masuala haya wapo makini kufanyia uchunguzi malighafi ya jezi hii. Tutakapolitambua tatizo tutatoa taarifa rasmi.”
Nyota wa Uswis Xherdan Shaqiri alisema, “Puma hawawezi kutengeneza kondom” baada ya mchezo wao dhidi ya Ufaransa kufuatia kushuhudia jezi za wachezaji wenzake wanne zikichanika. Puma ambao makao makuu yao yako nchini Ujerumani, walipata kashafa hiyo baada ya jezi za wachezaji wa Uswis Breel Embolo, Granit Xhaka, Admir Mehmedi na Blerim Dzemaili kuchanika katika mchezo wa juzi dhidi ya Ufaransa uliomalizika kwa suluhu.
Jarida la Blick linadai kwamba kuchanika huko kwa jezi kunatokana na
kuzidi kwa joto kwenye matengenezo ya jezi hizo hasa kwenye sehemu ya
namba na majina. Moja ya wachuuzi wa jezi za Puma nchini Uswis Ramon
Serrano amesema, “Ilionekana dhahiri kwamba sehemu ya namba katika
jezi ilikuwa imejichora sana kiasi ya kuwa hatarini kuchanika. Hasa
ukiangalia kwa upande wa Xhaka na Embolo, ilikuwa ni ushahidi tosha
kabisa. Kwa kuzichapisha kwenye zaidi ya nyuzi joto 150, lazima kutakuwa
na ‘chemical reaction’. Kwa kuongezea tu ni kwamba, ukiangalia jezi
zenyewe zinabana sana. Tisheti hazivutiki na kutanuka vizuri kama hapo
awali.”
CHANZO:MERIDIANI
0 comments:
Post a Comment