Paris,Ufaransa.
TIMU za taifa za Poland na Ujerumani zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya jioni ya leo kupata ushindi dhidi ya timu za taifa za Ukraine na Ireland Kaskazini.
Poland ikiwa katika uwanja wa Stade Verodrome,imeifunga Ukraine kwa bao 1-0 kwa bao la dakika ya 54 la winga Jakub Blaszczykowski.
Katika mchezo mwingine wa Kundi C uliochezwa katika uwanja wa Parc des Princes, Ujerumani imeichapa Ireland Kaskazini kwa bao 1-0 la dakika ya 29 la mshambuliaji Mario Gomez.
Germany: Manuel Neuer, Joshua Kimmich,Jerome Boateng, Mats Hummels, Jonas Hector, Sami Khedira, Toni Kroos, Mesut Ozil,Mario Goetze, Thomas Mueller, Mario Gomez.
Northern Ireland: Michael McGovern, Aaron Hughes, Craig Cathcart, Gareth McAuley,Jonny Evans, Jamie Ward, Corry Evans, Steven Davis, Oliver Norwood, Stuart Dallas, Conor Washington.
Kwa matokeo hayo Poland na Ujerumani kwa pamoja zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 baada ya kufikisha alama saba kila moja kufuatia kucheza michezo mitatu.
0 comments:
Post a Comment