Marc Wilmots
Lille ,Ufaransa.
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji,Marc Wilmots, ametangaza kuwa mlinzi wa timu hiyo,Jan Vertonghen hatacheza michezo yote iliyobaki ya Euro 2016 baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Jan Vertonghen
Vertonghen,25,amepata jeraha hilo leo jioni wakati alipokuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Ubelgiji kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Wales na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane.
Kuumia kwa Vertonghen ni pigo kwa Kocha Wilmots kwani alitegemea kumtumia mlinzi huyo katikati kuziba nafasi ya mlinzi mwingine wa timu hiyo Thomas Vermaelen anayetumikia adhabu.
Hii ina maana kwamba,Wilmots, sasa atalazimika kuwatumia Jason Denayer,Toby Alderweireld pamoja na Jordan Lukaku katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Wales.
0 comments:
Post a Comment