Marseille, Ufaransa.
URENO imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya usiku huu kuifunga Poland kwa penati 5-3 katika mchezo mkali wa robo fainali uliocheza katika uwanja wa Stade Vélodrome huko Marseille.
Mwamuzi aliamuru timu hizo zipigiane penati kumpata mshindi baada ya kwenda sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida na ule wa nyongeza.
Poland ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Robert Rewandowski kufunga dakika ya 2 akiunganisha krosi ya Kamil Grosick toka wingi ya kushoto.Ureno ilisawazisha dakika ya 33 baada ya Renato Sanchez kufunga kwa shuti kali akimalizia pasi ya kisigino kutoka kwa Louis Nani.
Ureno imepata penati zake kupitia kwa Ronaldo,Renato Sanches,João Moutinho,Luis Nani na Ricardo Quaresma aliyefunga penati ya ushindi.Penati za Poland zimefungwa na Lewandowski,Milik,Glik huku Jakub Blaszczykowski akikosa penati yake baada ya kipa wa Ureno,Rui Patricio kuipangua.
0 comments:
Post a Comment