728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 25, 2016

    ARSENAL YAPAA MAREKANI BILA YA NYOTA WAKE SABA WA KIKOSI CHA KWANZA

    London, England.

    KIKOSI cha wachezaji 24 cha Arsenal kimeondoka London mchana wa leo kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya ziara ya michezo ya kujipima nguvu tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England na michuano mingine.

    Katika ziara hiyo Arsenal imewaacha nyota wake saba wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa (majeruhi) na uchovu.

    Nyota walioachwa kutokana na uchovu ni Olivier Giroud,Laurent Koscienly,Mesut Ozil ,Alexis Sanchez ambao walikuwa wakizitumikia timu zao za taifa katika michuano ya Euro na Copa America.

    Danny Welbeck,Per Mertesacker na Gabriel Paulista wameachwa kutokana na kuwa majeruhi huku nyota wapya waliosajiliwa hivi karibuni na klabu hiyo Rob Holding na Granit Xhaka wakijumuishwa katika kikosi kilichosafiri mchana wa leo.

    Ikiwa nchini Marekani Arsenal itacheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki.Katika mchezo wa kwanza Arsenal itacheza na kombaini ya wachezaji wanaocheza ligi kuu ya Marekani maarufu kama MLS All-Stars huko San Jose siku ya Alhamis.

    Katika mchezo wa pili utakaochezwa siku ya Jumapili Arsenal itavaana na Chivas ya Mexico katika mji wa Los Angeles.

    Kikosi kamili kilichosafiri ni pamoja na:

    Makipa: Cech, Ospina,Martinez

    Mabeki: Debuchy, Monreal, Holding,Bellerin, Chambers, Gibbs

    Viungo: Coquelin, Bielik, Elneny,Wilshere, Iwobi, Xhaka, Cazorla, Zelalem,
    Reine-Adelaide, Oxlade-Chamberlain,Walcott

    Washambuliaji: Willock, Campbell,Akpom

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAPAA MAREKANI BILA YA NYOTA WAKE SABA WA KIKOSI CHA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top