Mauro Icardi
Icardi:Inter Milan imefungua milango kwa mshambuliaji na nahodha wake Mauro Icardi,23,kujiunga na Arsenal hii ni baada ya staa huyo wa Argentina kuripotiwa kuwa na mpango wa kugoma kujihusisha na masuala mbalimbali yaihusuyo klabu hiyo.(Daily Star)
Bonucci:Baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo,Paul Labile Pogba, Manchester United inajiandaa kubisha hodi kwa mara nyingine tena katika klabu ya Juventus kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati wa Italia,Leonardo Bonucci,29, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya £60m.(Daily Mirror)
Evans:Arsenal imeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili mlinzi wa kati wa zamani wa Manchester United, Jonny Evans,28,anayepatikana kwa dau la £16m na mlinzi wa Swansea City,Federico Fernandez,27,mwenye thamini ya £10m ili kuchukua nafasi ya Per Mertesacker,31,aliyeumia.(The Daily Mail)
Bulka:Chelsea imeripotiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuinasa saini ya Mlinda Mlango Kinda wa Poland,Marcin Bulka.(The Sun on Sunday)
Sigurdsson:Gylfi Sigurdsson yuko tayari kuikataa ofa ya kujiunga na Everton na kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Swansea City.(The Sun on Sunday)
Arias:Chelsea inapanga kufanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili Mlinzi wa kulia wa
Colombia,Santiago Arias.(The Sun on Sunday)
Milner:Kiungo wa Liverpool,James Milner,anafikiria kustaafu kuichezea England na katika kuhakikisha mpango huo unafanikiwa,tayari ametipotiwa kuwa wiki ijayo atakutana na kocha Sam Allardyce ili kulizungumzia suala hilo.(Sunday Telegraph)
Fellaini:Kocha mpya wa Sunderland,David Moyes, amepanga kuwasajili kwa mkopo Marouane Fellaini na Adnan Januzaj kutoka katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.(Sunday Mirror)
Flanagan:Mlinzi kinda wa Liverpool,Jon Flanagan,amekubali kujiunga kwa mkopo wa msimu mmoja na klabu ya Burnley ambayo imepanda ligi kuu England.(Sunday Mirror)
Bailly:Mlinzi mpya wa Manchester United,Eric Bailly,amesema kuwa alichagua kujiunga na klabu hiyo na siyo wapinzani wao wakubwa Manchester City baada ya kushauriwa na Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea,Didier
Drogba.(The Sun on Sunday)
Leiva:Kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29,wiki ijayo anatarajiwa kukamilisha usajili wa kujiunga na Galatasaray kwa ada ya uhamisho ya £2.3m.(Milliyet)
Ayew:West Ham United iko tayari kutoa dau la £20m ili kumsajili winga wa Swansea City,Mghana Andre Ayew.(Mail on Sunday)
Williams:Swansea City imekubali kumuuza mlinzi na nahodha wake Ashley Williams, 31, kwenda Everton kwa dau la £10m.(Sunday People)
Rahman:Mlinzi wa kushoto wa Chelsea Baba Rahman, 22,amesafiri kuelekea nchini Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Schalke kwa uhamisho mkopo wa msimu mmoja wenye makubaliano ya kuwa wa kudumu ikiwa atafanya vizuri.(London Evening Standard)
Augustinsson:West Ham inakaribia kumnasa mlinzi wa kushoto wa Sweden, Ludwig Augustinsson,22,kutoka FC Copenhagen kwa ada ya £5m ili kuziba pengo la mlinzi wake majeruhi,Aaron Cresswell.(Sunday Mirror)
Jesus:Manchester City imekubali kutoa dau la €32m ili kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras,Gabriel Jesus,18.(Globoesporte)
0 comments:
Post a Comment