728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 28, 2016

    CHELSEA PUNGUFU YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 ICC

    Pasadena,Marekani.

    IKICHEZA pungufu baada ya kiungo wake Cesc Fabregas kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya,Chelsea imeilaza Liverpool kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya International Champions Cup uliochezwa asubuhi ya leo katika uwanja wa Rose Bowl Pasadena,Marekani.

    Bao pekee la mchezo huo limefungwa kwa kichwa dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza na mlinzi Garry Cahill.Cahill amefunga bao hilo akimalizia kona safi ya Cesc Fabregas ambaye dakika ya 70 alilimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mlinzi wa kati wa Liverpool,Klavan.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA PUNGUFU YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 ICC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top