728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 26, 2016

    SPURS HOI MICHUANO YA ICC YACHAPWA 2-1 NA JUVENTUS

    Melbourne,Australia.

    MABAO mawili ya kipindi cha kwanza ya Mshambuliaji Paulo Dybala na Mlinzi Mehdi Benatia yameiwezesha Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya International Champions Cup uliofanyika mchana wa leo katika dimba la Melbourne Cricket Ground huko Melbourne,Australia.

    Tottenham Hotspurs ilijikuta ikikubali wavu wake uguswe baada Paulo Dybala kuifungia Juventus bao la kuongoza dakika ya 6 ya mchezo baada ya mlinzi Dominic Ball kufanya makosa na kupokonya mpira na Roberto Pereyra aliyetoa pasi kwa mfungaji.

    Dakika ya 14 Mehdi Benatia aliifungia Juventus bao la pili na kuifanya miamba hiyo ya Italia iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao hayo mawili.

    Mabadiliko yaliyofanywa mwanzoni mwa kipindi cha pili na Kocha Mauricio Pochetino yalionekana kuipa nguvu Tottenham Hotspurs kwani iliamka na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 67 kupitia kwa winga wake Erik Lamela.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SPURS HOI MICHUANO YA ICC YACHAPWA 2-1 NA JUVENTUS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top