728x90 AdSpace

Friday, July 22, 2016

LIVERPOOL YAMNYAKUA KIUNGO WA NEWCASTLE UNITED

Liverpool,England.

LIVERPOOL imemfanikiwa kumsajili kiungo,Mholanzi Georginio Wijnaldum,kutoka Newcastle United kwa ada ya uhamisho ya £25m.

Wijnaldum,25,amesaini mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa mshahara wa £75,000 kwa wiki.

Wijnaldum alijiunga na Newcastle mwaka jana kwa ada ya uhamisho ya 14.5m akitokea PSV Eindhoven ya nyumbani kwao Uholanzi.Akiwa na Newcastle Wijnaldum alifanikiwa kufunga mabao 11 na kutengeneza mengine matano katika michezo 38.

Wijnaldum anakuwa mchezaji wa saba kujiunga na Liverpool katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya Loris Karius, Joel Matip, Marko Grujic, Sadio Mane, Ragnar Klavan na Alex Manninger na atakuwa akivalia jezi namba 5 iliyokuwa ikivaliwa nahodha msaidizi wa zamani,Daniel Agger.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: LIVERPOOL YAMNYAKUA KIUNGO WA NEWCASTLE UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown