London, England.
ARSENAL imekamilisha usajili wa Mlinzi wa England,Rob Holding,kutoka Bolton Wanderers kwa ada ya Paundi Milioni mbili.
Holding,20,mwenye uwezo wa kucheza kama Mlinzi wa Kati na pembeni amesaini Mkataba wa Muda mrefu wa Kuichezea Arsenal baada ya mapema wiki hii Kufuzu vipimo vyake vya Afya.
Holding anakuwa Mchezaji wa Tatu kujiunga na Arsenal katika Kipindi hiki cha Usajili barani Ulaya.Wengine ni Granit Xhaka na Takuma Asano.
Msimu uliopita Holding aliichezea Bolton michezo 30 na kutangazwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment